BERLIN:Kuta la Berlin !
13 Agosti 2006Matangazo
Wajerumani leo wanaadhimisha siku ambapo kuta la Berlin lilijengwa miaka 45 iliyopita.
Maadhimisho hayo hasa ni ya kuwakumbuka watu 192 waliokufa wakati wakijaribu kuruka kuta hilo kutokea Berlin ya mashariki yatahudhuriwa na meya wa mji wa Berlin Klaus Wowereit na waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani bwana Wolgang Schäuble.
Ukuta wa Berlin ulioanza kujengwa usiku wa tarehe 13 mwezi agosti miaka 45 iliyopita uliutenganisha mji wa Berlin Magharibi na Ujerumani yote ya Magharibi.
Ukuta huo uliondoshwa mnamo mwaka 1990 baada ya mfumo wa kikomunisti kusambaratika katika Ulaya ya Mashariki.