BERLIN:Kansela wa Ujerumani aionya Iran juu ya kurejea tena na shughuli za kinuklia.
2 Agosti 2005Matangazo
Nae Kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder leo ameionya Iran juu ya uamuzi wake wa kurejea tena shughuli zake za kinuklia na kusema kuwa mataifa ya Magharibi kamwe hayatagawanyika katika msimamo wake kupinga mpango wa Tehran kuunda vbomu la atomiki.
Kansela Schroeder ambaye alikuwa akipokea tuzo ya amani kutoka kwa shirika moja la kujitolea la Ujerumani,amesema Umoja wa Ulaya ulikuwa tayari kutoa vivutio vikubwa vya kiuchumi iwapo serikali ya Iran ingekuwa imeonesha jitahada kubwa za kuumaliza mzozo aliouita mgumu na tete.