BERLIN:Jeshi la Ujerumani kuongeza muda wa kubakia Afghanistan kwa mwaka mmoja.
21 Septemba 2005Matangazo
Serikali ya sasa ya Ujerumani imesema inataka kuendelea kwa kipindi cha mwaka mmoja,kubakisha vikosi vya jeshi lake-Bundeswehr,nchini Afghanistan.
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Peter Struck,amesema idadi ya wanajeshi wa Ujerumani itaongezwa kwa askari 750 na kufanya kikosi kizima kuwa na wanajeshi 3000.Amesema wanajeshi hao wanaofanya kazi chini ya jeshi la Kimataifa,wamesaidia kuwezesha kufanyika uchaguzi ulio huru na wa haki wa bunge nchini Afghanistan kwa mara ya kwanza katika miongo kadhaa iliyopita.
Madaraka ya vikosi vinavyofanya kazi kama sehemu ya jeshi la Umoja wa Mataifa kusini mwa Sudan pia yanatazamiwa kuongezwa.Uamuzi huo unatazamiwa kuidhinishwa na bunge wakati litakapokaa katika kikao maalum wiki ijayo.