BERLIN:Chama kipya cha mlengo wa kushoto chaundwa Ujerumani
17 Juni 2007Matangazo
Chama kipya cha mlengo wa kushoto kilichoundwa jana nchini Ujerumani kimeshutumiwa vikali na wanasiasa wa vyama vya kiliberali na SPD.
Mwenyekiti wa chama cha kiliberali bwana Westerwelle amesema kuwa chama hicho kipya ni tishio kwa Ujerumani.
Chama hicho kipya ni zao la muungano wa vyama viwili vya mlengo wa kushoto kutoka Ujerumani magharibi na mashariki.