BERLIN:Baraza la mawaziri wakuu wa Ujerumani laidhinisha mageuzi katika mfumo wa shirikisho
7 Julai 2006Matangazo
Baraza la mawaziri wakuu wa Ujerumani limeidhinisha ,takriban kwa kauli moja mageuzi, katika mfumo wa shirikisho ambao umekuwa unatumika tokea mwaka 1949 hapa nchini.
Mageuzi hayo ni juu ya ugawaji wa mamlaka baina ya serikali kuu mjini Berlin na serikali za majimbo yote 16 ya Ujerumani.
Lengo kuu la mabadiliko hayo ni kuoanisha mchakato wa kupitisha maamuzi na sheria kwenye bunge.Chini ya mabadiliko hayo, serikali za majimbo zitakuwa na mamlaka zaidi ya kuamua juu ya saa za kazi,mambo ya elimu na juu ya usimamizi wa magereza