BERLIN
15 Februari 2005Serikali ya Ujerumani imo mbioni kimsingi kuchangia wanajeshi wake katika jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani litakalopelekwa nchini Sudan.Msemaji wa serikali amesema mjini Berlin kuwa umamuzi huo umetokana na maombi ya Umoja wa Mataifa kwa nchi zote wanachama kuchangia wanajeshi wa kulinda amani kwa ajili ya maeneo ya kusini mwa Sudan.
Hii imefuatia Marekani kusambaza azimio ambalo linataka utekelezwaji wa mpango wa kuweka silaha chini uliotiwa saini mwezi uliopita,ambao ulimaliza miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan.
Hata hivyo serikali ya Ujerumani imesema kabla haijapeleka wanajeshi wake,Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halina budi kupitisha azimio litakaloweka bayana uundwaji wa vikosi vya kulinda amani.
Kwa taratibu za Ujerumani,kwa jeshi lake kushiriki katika shughuli zozote za kimataifa ni lazima lipate idhini ya Bunge.