BERLIN
16 Februari 2005Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani,Joschka Fischer amekiri kuwa huenda alifanya makosa katika kushughulikia kile ambacho baadae kikaja kujulikana kama utaratibu legevu wa kutoa viza.
Akizungumza katika maojiano ya televisheni,Bwana Fischer amesema iwapo yeye binafsi ama wafanyakazi wa Wizara yake wamefanya makosa,basi anachukua jukumu la kuwajibika.
Wakati huo huo ripoti iliyotolewa na gazeti moja la mjini Munich iliyosema kuwa Waziri huyo alijua mapema uzembe huo kabla hajakiri,imekanushwa na Bwana Fischer mwenyewe.
Upande wa upinzani wa- waconsevativ unadai kuwa amri zilizokuwa zikitolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani,zimesaidia maelfu ya wahamiaji haramu kutoka mataifa ya Ulaya ya mashariki kuingia nchini,wengi kati yao wakisaidiwa na vikundi vya kihalifu.