BERLIN
25 Mei 2005Matangazo
Waziri mdogo wa mazingira wa Kenya, Bi Wangari Maathai, ambaye pia ni mshindi wa tunzo ya Nobel akiwa ziarani mjini Berlin hapa Ujerumani, ametoa mwito wa kutolewa misaada ya maendeleo iliyo madhubuti,. kupunguziwa madeni na kuweko mfumo wa haki wa biashara na Afrika.
Katika mkutano na waandishi habari alitaka nchi zilizoendelea kiviwanda zitoe fedha kwa wingi katika kuyatekeleza malengo ya Milenium ya kuupunguza umaskini kwa asilimia 50 duniani kote. Kati ya malengo hayo pia ni kuyafuta madeni ya mataifa yaliyo maskini kabisa duniani.
Maathai alisema lazima jitihada kubwa zaidi zifanywe ili kuweko mfumo wa haki wa biashara duniani, jambo ambalo ni muhimu kwa bara la Afrika.