BERLIN: Yushchenko ziarani Ujerumani
9 Machi 2005Matangazo
.
Rais wa Ukraine Viktor Yushchenko yuko mjini Berlin katika siku yake ya pili ya ziara yake rasmi nchini Ujerumani. Alitarajiwa leo kukutana na kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder na kuwa na mazungumzo na kiongozi wa chama cha upinzani Bibi Angela Merkel.
Yushchenko pia anatarajiwa kulihutubia bunge leo.
Wakati wa ziara yake hiyo , kiongozi huyo wa Ukraine amelenga katika lengo la kuiingiza nchi yake katika jumuiya ya Ulaya .Licha ya kile kinachoonekana kuwa kashfa ya viza , inayouhusu ubalozi wa Ujerumani nchini mwake, Yushchenko amesisitiza kuwa mahusiano ya nchi hizo mbili hayakuathirika.