BERLIN: Yushchenko kulihotubia bunge la Ujerumani
9 Machi 2005Matangazo
Rais Viktor Yushchenko wa Ukraine amesisitiza lengo lake la kutaka kuiongoza nchi yake kuwa mwanachama katika Umoja wa Ulaya.Ametoa tangazo hilo katika mahojiano yake na Redio Deutsche Welle,baada ya kuwa na mazungumzo pamoja na Rais Horst Köhler wa Ujerumani mjini Berlin.Rais Köhler alimpongeza Yushchenko kwa uchaguzi huru na wa haki uliomtia madarakani.Yushchenko alikutana vile vile na waziri wa kigeni wa Ujerumani Joschka Fischer.Hii leo Yushchenko mbali na kukutana na Kansela Gerhard Schroeder atatoa pia hotuba katika Bunge la Ujerumani mjini Berlin.