BERLIN; Wazri Fischer asema mapambano yanaendelea
10 Julai 2005Matangazo
Chama cha kijani kimesema kinadhamiria kupita katika uchaguzi mkuu ujao na hivyo kuweza kushiriki tena katika serikali ya Ujerumani.
Dhamira hiyo imesisitizwa na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani bwana Joschka Fischer kwenye mkutano wa chama hicho unaoendelea mjini Berlin.
Bwana Fischer amewataka wanachama wa chama chake waendeshe kampeni ya nguvu, na kwamba hakuna sababu ya kushika tama.
Chama cha kijani kimo katika serikali ya mseto na chama cha SPD cha Kansela Gerhard Schröder.
,