BERLIN: Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Joschka Fischer ...
12 Novemba 2003Matangazo
ametaka Urussi kuheshimu haki za kibinaadam katika Chechnya. Urussi, ikiwa ni mwanachama wa Baraza la Ulaya ambalo lina viwango vyake, inawajabika kutukuza hayo katika Chechnya, - alitamka Fischer kwenye jukwaa la majadiliano katika Radio Ujerumani mjini Berlin. Hakuna mtu anayeunga mkono kumegeka kwa ardhi ya Urussi. Wachechnya ni wakaazi wa Urussi ambao wanahitaji kulindwa kikamilifu na hasa kuhusika na haki za binaadam, - alisisitiza Fischer. Katika Chechenya, ni suluhisho peke la kisiasa litasaidia na ambalo linakubaliwa pia na wakaazi wengi wa Jamhuri hiyo ya Kokasia.