BERLIN Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Joschka Fischer, atashuhudia kuhusu kashfa ya utoaji visa.
18 Februari 2005Kamati ya bunge la Ujerumani inayosikiliza ushahidi kuhusu kashfa ya utoaji visa za kusafiria imeamua kwamba waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Joschka Fische,r atashudhudia mbele ya kamati hiyo baada ya kufanyika uchaguzi wa mikoa mwezi Mei. Kamati hiyo ilikataa pendekezo lililotolewa na chama cha upinzani cha Christian Democratic, kwamba Fischer ashuhudie haraka iwezekanavyo. Waziri Fischer amesema atachukua dhamana kwa makosa yoyote yaliyofanywa katika wizara yake ambayo yaliyasaidia makundi ya kigaidi ya Ukraine kutumia visa za watalii kuwaleta wahamiaji haramu nchini Ujerumani. Wapinzani wa kikosavativ wanasema uamuzi wa wizara ya Fischer mwaka wa 1999 kulegeza sheria za utoaji visa kwa raia wa mataifa ya Urusi ya zamani, kulifungua milango kwa wahamiaji haramu kuhamia Ujerumani.