Berlin. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani azungumza na mwenzake wa Syria.
30 Agosti 2006Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amezungumza kwa simu na waziri mwenzake wa Syria, Walid al-Moualem, kwa mara ya kwanza tangu pale waziri huyo wa Ujerumani alipofuta ghafla ziara yake mjini Damascus.
Shirika la habari la Syria limesema kuwa mawaziri hao wawili walijadili jinsi Syria inavyoweza kutoa mchango wake muhimu katika kuimarisha amani katika eneo la kusini mwa Lebanon.
Wizara ya mambo ya kigeni mjini Berlin imethibitisha kuwa mawaziri hao wawili walizungumza lakini imesita kusema kile kilichojadiliwa.
Steinmeier alifuta ziara yake mjini Damascus hapo August 15 kufuatia hotuba ya rais wa Syria Bashar al-Assad ambapo alikisifu kikundi cha wanamgambo wa Hizbollah na kuieleza Israel kama maadui.