BERLIN: Waziri Tzipi Livni ziarani Ujerumani
28 Agosti 2006Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Israel Tzipi Livni akiwa ziarani nchini Ujerumani hii leo anakutana na waziri wa nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier.Baadae leo mchana anataraji pia kukutana na Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel. Mazungumzo yao hasa yatahusika na mchango wa kijeshi unaotazamiwa kutolewa na Ujerumani katika vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Lebanon. Israel inashinikiza kuwa vikosi hivyo vipelekwe upesi iwezekanavyo,kusimamia makubaliano ya kusitisha mapigano yaliopatikana majuma mawili ya nyuma.