BERLIN Waziri Schilly ashuhudia mbele ya tume ya bunge inayochunguza kashfa ya utoaji visa
16 Julai 2005Matangazo
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani bwana Otto Schilly, alihojiwa jana na kamati maalumu ya bunge inayochunguza kashfa ya utoaji visa. Kuzilegeza sheria za utoaji visa kulisababisha idadi kubwa ya wahamiaji wasio halali kuingia Ujerumani kutoka Ulaya Mashariki.
Kwa zaidi ya saa 15, waziri Schilly alishuhudia na kukanusha madai kwamba alifanya makosa katika kashfa hiyo. Alisema wizara ya mambo ya kigeni ndiyo iliyokuwa na jukumu la kutoa visa za kusafiria.
Wanasiasa wa upinzani wanataka kujua ikiwa waziri Schilly alifahamu kuhusu kutumiwa vibaya kwa visa hizo na kwa nini serikali ilishindwa kuchukua hatua.