Berlin: Waziri mdogo wa Ujerumani wa ushirikiano wa kiuchumi, Bibi Uschi...
27 Novemba 2003Matangazo
Eid, katika mashauriano baina ya serekali ya Ujerumani na Rwanda, yaliomalizika mjini Bonn jana, aliiahidi nchi hiyo ya Kiafrika kwamba Ujerumani itashirikiana nayo katika mpango wake wa kupeleka madaraka mikoani, kujenga misingi ya huduma za afya na kupambana na UKIMWI pamoja na kuleta marekebisho ya kiuchumi na kujenga mfumo wa uchumi unaotegemea masoko. Katika kusaidia kupamnana na athari za mauaji ya kiholela yaliotokea nchini humo, serekali ya Ujerumani itaisaidia tume ya taifa ya upatanishi ya Rwanda, na pia kujenga mifumo ya mahakama.