BERLIN: Waziri Fischer aonya
21 Juni 2005Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani bwana Joschka Fischer ameonya dhidi ya kurudisha nyuma, hatua za kuupanuza Umoja wa Ulaya , baada ya kushindwa kwa mkutano mkuu wa viongozi wa Umoja huo mjini Brussels wiki jana.
Waziri Fischer amesema hayo kwenye mkutano na waandishi habari mjini Berlin na kuongeza kwamba bara la Ulaya linahitaji kuwa na zaidi ya soko la pamoja ili kudumisha amani na kulifanya liwe tengemavu.
Bwana Fischer pia ameeleza kwamba kushindwa kwa viongozi wa Ulaya kufikia mapatano juu ya bajeti ya Umoja wao kumesababishwa na ubinafsi na ukosefu wa mshikamano .
.