Berlin. Waziri ahojiwa masaa 15 kutokana na kashfa ya Visa.
16 Julai 2005Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani amekabiliwa jana na mahojiano ya muda mrefu katika uchunguzi wa bunge juu ya kashfa ya visa miaka mitano iliyopita, ambamo kulikuwa na wahamiaji kadha walioingia nchini kinyume na sheria kutoka Ulaya mashariki.
Kwa muda wa zaidi ya saa 15, Otto Schilly alikuwa akitoa ushahidi wake moja kwa moja akionekana katika televisheni na kukanusha madai kuwa alihusika na kashfa hiyo.
Amesema kuwa wizara ya mambo ya kigeni ndio inayohusika moja kwa moja kwa kutoa visa.
Kuanzia mwaka 1999 hadi 2000 hatua za kulegeza masharti ya upatikanaji wa visa ziliruhusu maelfu ya wafanyakazi kinyume na sheria kutoka Ukraine, ikiwa ni pamoja na wahalifu pamoja na wanawake wanaojiuza miili yao , kuingia nchini Ujerumani.
Chama cha upinzani cha Kihafidhina cha CDU, kina nia ya kutaka kujua iwapo Bwana Schily alijua taratibu hizo za matumizi mabaya ya visa na kwamba kwanini serikali ilishindwa kuchukua hatua.