BERLIN: Wataalamu wa Kijerumani wapelekwa Marekani
9 Septemba 2005Matangazo
Timu ya kiasi ya wataalamu 100 wa Kijerumani imepelekwa Marekani kusaidia katika maeneo yalioteketezwa na kimbunga Katrina.Kazi yao kubwa ni kuondoa maji ya mafuriko kwa kutumia pampu 15 zenye nguvu kubwa.Timu ya maafisa wa polisi kutoka Ujerumani pia inapelekwa Marekani kusaidia kazi ya kutambua maiti.Vile vile,serikali ya Ujerumani inakusudia kupeleka msaada mwengine wa tani 75 za chakula.