BERLIN: Washukiwa walikuwa na mawasiliano Ujerumani
13 Agosti 2006Matangazo
Afisa wa ngazi ya juu katika wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani amesema,baadhi ya watu waliokamatwa Uingereza siku ya Alkhamisi, wakishukiwa kuhusika na ugaidi walikuwa na mawasiliano nchini Ujerumani.Naibu waziri,August Hanning ameliambia gazeti la “Bild am Sonntag” kuwa Ujerumani haikulengwa katika njama iliyozuiliwa,ikisemekana azma ilikuwa ni kuripua ndege zinazokwenda Marekani kupitia bahari ya Atlantik.Hapo awali Pakistan ilimtaja raia wa Kingereza anaeshukiwa kuhusika na Al-Qaeda kama ni mtu muhimu katika njama hiyo.Serikali ya Uingereza inaendelea kupeleleza mpango huo unaosemekana kuwa ulipangwa na washukiwa waliokamatwa siku ya Alkhamisi.Mmoja kati wa washukiwa hao 24 ameachiliwa huru.