BERLIN. wanasiasa wataka mfumo wa usalama uchunguzwe upya
24 Julai 2005Matangazo
Viongozi wa kisiasa nchini Ujerumani wametoa wito wa kuchunguzwa upya mfumo wa usalama nchini humu baada ya ndege moja ndogo kuanguka katika uwanja wa bunge la Ujerumani Reichstag karibu na ofisi ya kansela Gerhard Schröder.
Ajali hiyo ilitokea siku ya ijumaa jioni wakati watu kadhaa walikuwa kwenye mlolongo wa kuingia kuzuru majengo ya bunge.
Rubani wa ndege hiyo alikufa papo hapo lakini hakuna mtu mwingine yeyote aliyeuwawa au kujeruhiwa.
Polisi mjini Berlin wamesema kuwa wameanzisha uchunguzi wa kilichosababisha ajali hiyo na wakati huo huo wamesema kuwa ajali hiyo haihusiani na kitendo cha kigaidi.
Usalama nchini Ujerumani umeimarishwa zaidi tangu kisa cha mashambulio ya mabomu nchini Uingereza.