BERLIN: Wajerumani wakimbia mashambulio ya Israel
16 Julai 2006Matangazo
Tangu siku ya Ijumaa,kiasi ya Wajerumani 200 wameondoka Lebanon kwa njia ya barabara.Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni mjini Berlin amearifu kuwa Wajerumani hao walipelekwa Syria katika msafara wa magari uliyotayarishwa na ubalozi wa Ujerumani mjini Beirut.Akaeleza kuwa wizara hiyo imeimarisha idadi ya wafanya kazi wake ubalozini kuwasaidia wale wanaojaribu kuyakimbia mashambulio ya angani ya Israel nchini Lebanon.Kabla ya mashambulio hayo,kiasi ya Wajerumani 1,100 walikuwa wakiishi Lebanon; miongoni mwao kiasi ya 500 wana uraia wa nchi mbili.