BERLIN Vitambulisho vipya kutolewa Ujerumani
23 Juni 2005Matangazo
Ujerumani imetangaza uamuzi wa kuanzisha kutoa vitambulisho vipya kaunzia mwezi Novemba mwaka huu. Tangazo hilo linafuatia pendekezo lililotolewa na waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani bwana Otto Schilly. Serikali inataraji kuboresha usalama na kukomesha udanganyifu. Gharama yake itakuwa euro 59, ikiwa ni mara mbili ya bei ya vitambulisho vya zamani.