BERLIN : Viongozi wafanya mdahalo wa mwisho wa uchaguzi
13 Septemba 2005
Nchini Ujerumani viongozi wa vyama vya kisiasa wamekuwa na mdahalo wao mkubwa wa mwisho kwenye televisheni kabla ya uchaguzi mkuu wa taifa uliopangwa kufanyika Jumapili.
Wakati wapiga kura wengi ikiwa bado hawakuamuwa nani wa kumpa kura zao ni vigumu kutabiri mmundo wa serikali mpya utakuwaje.Uchunguzi wa maoni unaonyesha kwamba kumeibuka kuungwa mkono kwa dakika za mwisho kwa chama cha Social Demokrat cha Gerhard Schroeder.Vyama vya kihafidhina bado vinaonekana kuwa vitaweza kusomba kura nyingi lakini yumkini ikawa zisitosehe kuviwezesha kuunda serikali ya mseto ya chaguo lao kwa kushirikiana na chama cha Free Demokrat.
Mdahalo huu ulikuwa ni wa pili kupitia televisheni kati ya Kansela Gerhard Schroeder na mpizani wake Angela Merkel kuelekea uchaguzi mkuu lakini safari hii viongozi wa vyama vidogo pia vilijiunga na mjadala wa mdahalo huo.