BERLIN : Viongozi wa Ujerumani wamtetea Papa
17 Septemba 2006Matangazo
Kansela Angela Merkel na viongozi wengine mashuhuri wa kisiasa nchini Ujerumani wametetea hotuba iliozusha utata ya Papa Benedikt wa 16 kuhusu Uislamu aliyoitowa wakati akiwa ziarani nchini Ujerumani hivi karibuni.
Akizungumza na gazeti la Ujerumani la Bild Merkel amesema matamshi hayo ya papa yameeleweka vibaya.
Naye kiongozi wa chama cha Christian Social Union Edmund Stoiber amesema haoni sababu ya kushutumu matamshi hayo ya papa.