BERLIN: Vikosi vya KSK vitabakia Afghanistan
21 Oktoba 2006Matangazo
Serikali ya Ujerumani imesema itaendelea kuvitumia vikosi vyake vya tabaka ya juu KSK nchini Afghanistan licha ya mfungwa aliekuwa jela ya Guantanamo Bay kudai kuwa aliteswa.Mwezi wa Agosti,Murat Kurnaz aliezaliwa Ujerumani na mwenye asili ya Kiturki,aliachiliwa kutoka jela ya kijeshi ya Marekani,Guantanamo Bay baada ya kuzuiliwa kwa miaka minne.Amedai kuwa alipozuiliwa na Wamarekani nchini Afghanistan, aliteswa na wanajeshi wa Kijerumani wa kikosi cha KSK.Msemaji wa serikali mjini Berlin amesema, hakuna mpango wa kuviondosha vikosi vya KSK kutoka Afghanistan.Akaongezea kuwa serikali,siku ya Jumatano inatazamia kurefusha mamlaka ya vikosi vya Kijerumani kupiga vita ugaidi nchini Afghanistan na kwa hivyo hata kikosi cha KSK kitabakia huko.