Berlin. Ukuaji wa uchumi wa Ujerumani utapungua.
22 Oktoba 2005Matangazo
Serikali ya Ujerumani imepunguza utabiri wake wa ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo kwa mwaka 2006.
Waziri wa uchumi anayeondoka katika wadhifa huo Wolfgang Clement ametangaza kuwa utabiri huo umepunguzwa hadi asilimia 1.2 kutoka asilimia 1.6 hapo kabla.
Clement amesema kuwa bei kubwa ya mafuta inakinza ukuaji wa uchumi.