Berlin: Ujeumani inaunga mkono kusamehewa madeni nchi maskini
6 Julai 2005Matangazo
Kansela Gerhard Schroader wa Ujerumani ameyatilia nguvu matakwa ya nchi maskini kabisa kusamehewa madeni. Katika makala alioyaandika katika gazeti la TAGESSPIEGEL la hapa Ujerumani, Kansela Schroader ametaka msamaha huo wa madeni ufungamanishwe na utawala bora katika nchi za Kiafrika. Inakadiriwa kwamba nchi zinazohusika zitaweza kusamehewa karibu ya Euro bilioni 47.