Berlin. Ujerumani yatakiwa kuongeza madaraka ya polisi.
26 Julai 2005Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Otto Schilly ametoa wito wa kuongeza madaraka ya polisi baada ya shambulio la mabomu nchini Misr, ambalo limesababisha watu 84 kuuwawa.
Katika mahojiano na gazeti la Bild, Schily amesema kuwa wachunguzi wanapaswa kupewa mamlaka zaidi na kuchukua hatua za dharura za ulinzi dhidi ya mashambulizi ya kigaidi.
Hatua hiyo itakuwa na maana ya kubadilisha katiba.
Schily pia ametoa wito wa kuanzishwa kwa sheria ya kuzuwia ndege kupita angani wakati wa ziara ya kiongozi wa kanisa Katoliki nchini Ujerumani mwezi August na wakati wa michezo ya fainali za kombe la dunia mwaka 2006.
Mapendekezo hayo yanakuja baada ya ndege ndogo kuanguka karibu na jengo la bunge la Ujerumani mjini Berlin siku ya Ijumaa.