Berlin. Ujerumani yashutumu mauaji ya waziri wa Sri lanka.
13 Agosti 2005Matangazo
Ujerumani ni moja kati ya nchi kadha zilizoshutumu mauaji ya aliyekuwa waziri wa mambo ya kigeni wa Sri Lanka Lakshman Kadirgamar.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Joschka Fischer amesema katika taarifa kuwa wauaji wa Kadirgamar ni lazima wafikishwe mbele ya sheria.
Amesema kuwa ametuma ujumbe kwa rais wa Sri Lanka Chandrika Kumaratunga akielezea masikitiko yake kwa familia ya waziri huyo pamoja na Wasri Lanka wote.
Fischer amemwelezea Kadirgamar kuwa ni rafiki wa Ujerumani na mzalendo ambaye alikuwa na heshima kubwa duniani kote.